Benki ya Exim yatangaza likizo ya malipo ya mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 160 kwa wateja wake ili kuwanusuru na athariza janga la COVID – 19.

Benki
ya Exim yatangaza likizo ya malipo ya mikopo yenye thamani ya Shilingi
bilioni 160 kwa wateja wake ili kuwanusuru na athari za janga la COVID –
19.
Benki
ya Exim imetangaza msamaha wa likizo ya malipo ya mikopo kwa wateja
wake wakubwa, wa kati na wadogo walipo katika sekta zilizo athirika
zaidi kiuchumi kutokana na athari za mlipuko wa ugonjwa wa virus vya
Corona (COVID 19). Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea
kuchukuliwa na benki hiyo katika kuwasaidia kifedha wateja wake waliopo
sekta ambazo zimeathiriwa zaidi na athari za mlipuko wa ugonjwa huo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki
ya Exim, Bw Jaffari Matundu alisema msamaha huo wenye thamani ya zaidi
ya sh Bilioni 160 umeanza mwezi Juni mwaka huu, ukihusisha likizo ya
malipo ya mikopo kwa wateja na nyongeza ya muda wa urejeshaji wa mikopo
ili kusaidia wateja wa benki hiyo katika sekta mbali mbali kutokana na
athari za janga hilo kwenye biashara zao.
“Benki
inaelewa mahitaji ya wateja wetu wakati huu na tunafanya yote
yanayowezekana kuwasaidia ili waweze kuvuka salama katika kipindi hiki
kigumu. Jitihada hizi haziishii tu kwenye misamaha hii tunayoitoa bali
pia kupitia huduma za ushauri kuhusu mikakati ya biashara ili
kuhakikisha kwamba biashara za wateja wetu zinadumu na zinafanyika kwa
mafanikio zaidi,” alisema.
Kwa
mujibu wa Bw Matundu msamaha huo unazingatia vigezo mbalimbali kwa kila
mteja kwa kuwa athari za COVID-19 hazikuwa sawa katika sekta zote.
“Tunafarijika kwa kuwa tayari wateja waliopo kwenye sekta zilizoathiriwa
zaidi wameshaanza kusaidiwa. Mazungumzo na wateja wengine bado
yanaendelea ili kutambua hatua mbali mbali zinazofaa kulingana na aina
ya biashara, ” aliongeza.
“Siku
zote Benki ya Exim, tunaamini katika kufanya kazi kwa bidii leo kwa
ajili ya kesho bora kwa wateja wetu, biashara zao na jamii kwa jumla, ni
kwa mtazamo huo tumepitisha hatua kama hii katika wakati huu
mgumu.Tunaendelea kujitolea kushughulikia mambo haya na kupata suluhisho
sambamba na mamlaka pamoja na Serikali katika kuhakikisha uchumi wetu
unaendelea kuwa thabiti wakati wa nyakati hizi ngumu. ” alihitimisha.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )