BENKI YA 1&M TANZANIA YATIA FORA SABASABA

Kutoka kushoto ni Mkuu
wa Huduma za Rejareja wa Benki ya I&M Tanzania, Lilian Mtali,
Meneja Masoko na Mawasiliano, Anitha Pallangyo, Ofisa Mauzo, Beatrice
Fusi, Meneja Mwandamizi (Madeni na Maendeleo ya Bidhaa), Deepali
Ramaiya, Meneja wa Tawi la Nyerere, Said Gagu na Ofisa Masoko na
Mawasiliano, Debora Mwakyoma wakiwa katika Maonyesho ya 44 ya Kimataifa
ya Biashara ya Sabasaba, Dar es Salaam.

 
Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

BENKI
ya I&M Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza Maonyesho ya 44 ya
Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, lakini inang’ara kwa kutoa bidhaa na
huduma za kipekee ambazo zinakidhi mahitaji yote ya mteja katika soko.

I&M
Tanzania ilitambulisha akaunti mpya ya wanawake ya Tunaweza inayotoa
suluhisho kwa wanawake wa ngazi zote kuanzia mmoja mmoja, wajasiriamali
hadi kikundi au taasisi.

Akaunti hiyo inajitofautisha kwa kutoa
huduma bila malipo yoyote, haina makato ya kila mwezi na viwango vyake
vya riba vinavutia kwenye akiba.

Akizungumza
leo jijini Dar es Salaa, katika maonyesho hayo, Meneja Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya I&M, Anitha Pallangyo, alisema kuwa bidhaa
hiyo mpya imeunganishwa kwenye mtandao wa benki wa kidijitali ili kuwapa
wateja huduma bora na endelevu wakati wowote wanapohitaji.

Amesema
I&M Tanzania ni sehemu ya I&M Holdings Kenya iliyoanzishwa
mwaka 1974 kama kampuni ya huduma za kifedha kabla baadaye kubadilishwa
kuwa benki ya biashara.

“Mwaka huu inasherehekea miaka kumi ya
huduma zetu katika soko la Tanzania. Tunafurahi kuendelea kuhudumia
wateja wetu na wateja wapya, pia tunashukuru wateja wetu na washikadau
wote walioshiriki katikakuiletea benki mafanikio makubwa kwa kipindi
chote cha miaka kumi kwenye soko.”

“Tunatoa huduma kadhaa za
kifedha ikiwa ni pamoja na akaunti ya akiba, current akaunti kwa
madhumuni ya biashara, mikopo ya biashara, huduma za kubadili fedha,
uhamishaji fedha kitaifa na kimataifa, huduma za kidijitali ambazo hutoa
fursa kwa mteja kupata huduma za benki kupitia simu za mkononi kwa
kupiga namba *150*32# au kupitia iClick- huduma ya benki kwa njia ya
mtandao inayopatikana bila kikomo kwa saa 24,” amesema Anitha

Meneja
Masoko na Mawasiliano huyo wa benki hiyo, amesema kuwa pia benki yao
wanatoa unafuu na urahisi wa kupata mikopo na huduma nyingine kadhaa
ambazo ziliwafanya watu waliotembelea banda lake kwenye maonyesho ya
Sabasaba lililopo ukumbi wa Karume, upande wa kulia wa lango la
kuingilia kuhamasika na kutaka kujua zaidi kuhusu benki hiyo.

“I&M
inafungua milango kwa Watanzania wote kwenda kujiunga na benki
inayojali mahitaji yao, iliyo tayari kuwapa huduma za kipekee za kifedha
kupitia wafanyakazi wake wenye uzoefu zaidi katika kutoa huduma bora
kwa wateja.

“Mbali na kushiriki katika maonyesho ya Sabasaba,
benki hiyo inatoa huduma zake bora kupitia mtandao wa matawi yake
yaliyoko maeneo ya Maktaba, Indira Gandhi, Nyerere, Kariakoo, Oysterbay
pamoja na mikoani ikiwa ni pamoja na Moshi, Arusha na Mwanza,” amesema


 Timu
ya wafanyakazi wa mauzo na idara ya masoko wa benki hiyo kutoka matawi
yake ya Dar es Salaam inayoongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa
Benki ya I&M, Anitha Pallangyo na Ofisa Masoko na Mawasiliano,
Debora Mwakyoma wapo kwenye maonyesho hayo ili kuwapa wageni na wale
ambao wanataka kuwekeza katika benki inayoaminika na salama ikiwa na
huduma za ATM zinazopatikana kwa saa 24.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )