Babalevo atangaza kugombea ubunge jimbo la Zitto

ImageMsanii Babalevo ambaye ni
diwani aliyemaliza muda wake katika kata ya Mwanga Kaskazini Manispaa ya Kigoma
Ujiji kupitia chama cha ACT wazalendo, amesema sasa anakwenda kugombea ubunge.
Babalevo amesema ni muda
sasa wa kuwania ubunge na atakwenda kugombea katika jimbo la Kigoma Mjini.

”Baada ya hapa naondoka naelekea Kigoma kwa
wananchi wangu nakwenda kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini
kama Mh Zitto hatagombea lakini akigombea nitaenda jimbo jingine”, amesema.

Babalevo amehudumu kama diwani wa Mwanga
Kaskazini kwa miaka mitano lakini pia amewahi kutumia kifongo jela, ambapo
mwenyewe anasema jela ilimfundisha mambo mengi ikiwemo kumjua Mungu.

Kwa upande mwingine Babalevo amesema akipata
kiinua mgongo chake cha Mil 20 au zaidi basi Mil 10 atazirudisha kwa wananchi
wake.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )