AYAC WAFUNGUA DIRISHA LA USAJILI WA MBIO ZA RIADHA KWA WATOTO.

Teddy Kilanga

Arusha Youth Athletics Championiship(AYAC) wamefungua dirisha la usajili wa mbio za riadha kwa watoto wa umri wa miaka sita hadi 14 ili kukuza vipaji katika tasnia ya mchezo huo.

Akizungumza muandaaji wa mashindano hayo kutoka taasisi hiyo yanayotarajiwa kufanyika mnamo machi 28 mwaka huu,Juliana Mwamsuva alisema madhumu yake nikuongeza ushiriki wa watoto katika michezo pamoja na kukuza kizazi chenye uelewe na kujenga taaluma ya mchezo wa riadha.

“Michezo mbalimbali ya riadha  nil ile ya mbio fupi na ndefu,kuruka vihunzi pamoja na vijiti na mashindano haya kwasababu yamegusa watoto wengi ambao wako mashuleni yaani wa shule za msingi na sekondari katika jiji la Arusha,”alisema Mwansuva.

Kwa upande wake Makamo wa rais wa chama cha riadha Tanzania,John Bayo alisema mbio za uwanjani zilikuwa hazijapewa kimpaumbele hivyo anashukuru Mwandaaji huyo kwa kuwekeza kwa watoto japo baadhi ya shule wanafanya kwa kiasi kidogo.

“Umri mzuri ni watoto wa miaka hiyo 6-17 ambaye atarithi na kuendelea kuhamasisha wengine pamoja nakumjengea uwezo wake kama sehemu ya maisha yake,”alisema.

Naye Katibu wa chama cha riadha wa halmashauri ya jiji la Arusha,Rogath Stephen alisema mashindano hayo yatajumuhisha mbio za mita 50 kwa watoto wa umri wa miaka sita kwa lengo la kuendeleza vipaji vya watoto kwani Tanzania imekuwa na uhaba wa wanariadha.

“Sisi tumekuwa hatuna chain ya kuwaandaa wanariadha wetu yani wale wanaoacha nafasi zao kwa kustaafu wawezo wakuziba hizo nafasi mfano nchi ya Kenya na Ethiopia ndio wanamfumo huo ndio maana wanaidadi ya wanariadha walioqualify kwenye michezo ya Olympic,”alisema Katibu huyo .

Alisema kwa kushirikiana na AYAC wameanza kuboresha hivyo wadau wengine wajitokeze katika kuunga mkoano michezo ya riadha hadi kufikia viwango vya Olympic hivyo wazazi wajitokeze kusajili watoto wao.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )