AY ALA SHAVU LA INFINIX NOTE 7 (BIGI MAKINI)


Msanii mkongwe katika industry ya muziki, “AY” anayetamba na kibao cha Danhela ala shavu la Ubalozi wa simu mpya ya Infinix NOTE 7.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, @infinixmobiletz waliweka viashiria vya ubalozi huo wiki iliyopita na siku ya Jumamosi, Mei 9 walithibitisha ubalozi huo kupitia LIVE Session ya Instagram iliyo onyesha wawakilishi wa Infinix wakifanya mazungumzo na AY kuhusiana na simu ya Infinix NOTE 7.
Infinix NOTE 7 imepewa jina la Bigi Makini, na ndio sababu kuu iliyopelekea Infinix kufanya kazi na AY, kwani wengi tunafahamu AY ni msanii mkongwe mwenye mafanikio makubwa mwenye kuheshimika kutokana na mchango wake katika game la muziki Tanzania.
Infinix NOTE 7 simu yenye umbo kubwa la inch 6.95 na speed ya ajabu ya G70 processor na kutokana na sifa hizi huenda Infinix NOTE 7 ndiyo simu yenye uwezo mkubwa na yenye kuvutia zaidi kwa mwaka huu wa 2020.
Ili kufahamu mengi zaidi kuhusiana na Infinix NOTE 7 na bidhaa nyengine za Infinix tafadhali tembelea kurasa zao za mitandao ya kijamii @infinixmobiletz

Kind regards
Alex Mathias Sonna
Chief Editor Fullshangwe Blog
Email:[email protected]
Cellphone:+255653257072
Twitter:@ALEXSonna
Instagram:@sonnaalex

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus (0 )