AUDATS KISATO AJITOSA UBUNGE JIMBO LA NKASI KUSINI-Awaomba wananchi kumuombea katika nia yake hiyo

NA ANDREW CHALE

KADA wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Audats Salvatory Kisato ametangaza nia kuomba ridhaa ya kugombea Kiti cha Ubunge Jimbo la Nkasi Kusini ili kuondoa changamoto na kero za muda mrefu ndani ya jimbo hilo.

Kisato anaeleza kuwa ni wakati sasa wa kuleta mabadiliko ya dhati na dhamira ya kweli na anaamini aliyekuwepo awali aliongoza jimbo hilo kwa vipindi viwili anahitaji kupokelewa kijiti.

“Nina nia ya dhati ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Nkasi Kusini, maombi yenu muhimu sana ndugu jamaa na marafiki na wana Nkasi wote”. Alisema Kisato

Na kuongeza kuwa:
                                 “Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha kuwa, nimekusudia kutangaza nia ikiwemo na kuomba ridhaa ya kugombea Kiti cha nafasi ya Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Nkasi Kusini” Alisema Kisato.

Akielezea kwa kina kwa nini atangaze nia ya kugombea jimbo hilo la Nkasi Kusini lililopo Mkoa wa Rukwa, alieleza:

“Nimeziona changamoto za Wana Nkasi na kwa uzoefu nilionao wa kutumikia jamii naona natosha kuzikabili changamoto hizo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.” Anasema Kisato

Kisato anasema kuwa nia yake hiyo endapo atapata nafasi basi atahakikisha Jimbo la Nkasi linakuwa na Mbunge makini ambaye atawasemea kikamilifu changamoto za WanaNkasi pindi atakapopata ridhaa ya kuwa Mbunge na ikiwemo kuhakikisha Nkasi inapata maendeleo ya endelevu na ikiwemo kufikiwa na huduma za kijamii kwa haraka kulingana na kasi inayotokana na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

“Nitakuwa kiungo makini ambaye nitawaunganisha vyema ikiwemo na kuboresha Umoja, Mshikamano na Ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini na CCM pamoja na Serikali.

..nikiwa na lengo la kutumia muunganiko huu kuhakikisha Nkasi Kusini inakuwa na Maendeleo thabiti yasiyo legalega.” Anasema Kisato

“Nitatumia Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhakikisha Nkasi Kusini inakuwa na maendeleo sawa ukilinganisha na majinbo mengine yaliyoendelea ikiwemo kuitangaza vyema Nkasi kwa wadau wa maendeleo ikiwemo taasisi za maendeleo za kimataifa.”  Anasema Kisato.

“Kumsaidia Mhe. Dkt, John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Safari ya kuijenga Tanzania Mpya yenye maendeleo endelevu kwa ujumla ikiwemo na Jimbo la Nkasi Kusini.” Anasema Kisato.

“Ninaamini kwa imani yangu endapo nitapewa ridhaa hii nitafaa kuliongoza Jimbo la Nkasi Kusini kwa kufata miongozo iliyopo kwenye Ilani ya CCM ikiwemo kufanya kazi kwa bidii kulingana na kasi anayoenda nayo Dkt, John Pombe Magufuli.” Anasema Kisato.

Kisato anabainisha kuwa hili kufikia malengo hayo ameomba kuombewa ili kupata kibali.    

“Mniombee ili nipate kibali cha kupitishwa kwenye Kura za maoni.
Ninaomba ‘Support’ zenu Ndugu zangu ili niweze kutimiza lengo hili kwa maendeleo ya WanaNkasi Kusini” Alieleza Kisato.

“Mimi kijana wenu Mpendwa na Mtumishi wenu Audats Salvatory Kisato. Ahsante sana na MUNGU awabariki sana” Alimalizia.

Wasifu wake hadi sasa Kisato ana umri wa miaka 37 Mzaliwa wa Nkasi Mkoani Rukwa, kabira Mfipa.

Uzoefu wake kwenye Chama: Katibu Wilaya Tandahimba CCM, Mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Arusha Mjini – akiwakilisha tawi la Engira.

Kielimu:
Shahada ya Uchumi Mzumbe 2005/2008
– Shahada ya Uzamili na Utawala na Raislimali watu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM ).

-Amesajili: Chuo Kikuu Ardhi, Shahada ya Uzamivu ya Utungaji wa Sera na usimamizi wa program.

Uzoefu wa kikazi:
Muwezeshaji wa TAFES Kanda ya Kaskalzini 2008/2009
– Muwezeshaji katika shirika la Compassion International Tanzania kwa zaidi ya miaka 11hadi sasa.
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )