ASKOFU MAPUNDA ATAKA UPENDO, HURUMA NA MSAMAHA VIDUMISHWE

 Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda (aliyevaa kofia) akiwa amelala kifudifudi na mapadre wengine ikiwa ni ishara ya unyenyekevu kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani hapa jana.
 Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda akiongoza waumini wa kanisa Katoliki kuabudu msalaba kwenye ibada hiyo.
 Tendo la kuabudu msalaba likiendelea.
 Tendo la kuabudu msalaba likiendelea.
 Tendo la kuabudu msalaba likiendelea.
 Tendo la kuabudu msalaba likiendelea.
 Tendo la kuabudu msalaba likiendelea.
  Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda, akihubiri kwenye ibada hiyo.
  Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda (katikati) akiwa na mapadre wengine wakiongoza kipengele cha sala za waamini kwenye ibada hiyo. ‘Simameni….pigeni magoti’.
 Ibada  ikiendelea.
 Ibada  ikiendelea.
 Ibada  ikiendelea.
 Ibada  ikiendelea.
 Ibada  ikiendelea.
 Waumini wakinawa mikono kama tahadhari ya kujikinga na mlipuko wa maambukizi ya Virusi vya Corona kabla ya kuingia kanisani kuanza Ibada ya Ijumaa Kuu.

Ibada  ikiendelea.
Na Godwin Myovela, Singida

Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda amewataka waumini wa dhehebu hilo daima kuwa vyombo vya upendo, huruma na msamaha kama kumbukizi na tafakuri halisi ya Ijumaa Kuu katika muktadha chanya wa kumuishi Yesu Kristu kwa matendo.

Mapunda amesema kuendelea kutendeana vitendo vya kikatili, kutosameheana sisi kwa sisi, kupakaziana na kubambikiana kesi, sambamba na kuchafuana kwa namna yoyote ile ni kuendelea kumsulubisha Yesu Kristu msalabani.

Mhashamu Askofu Mapunda aliyasema hayo wakati akiongoza mamia ya waumini wa kanisa katoliki walioshiriki ibada ya Ijumaa Kuu kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu, mkoani hapa.

” Tusitendeane vitendo vya kikatili, na daima tuwe vyombo vya upendo, huruma na msamaha,” alisema Mapunda na kuongeza:

” Kifo hiki cha Kristu kinatufubdisha upendo wa kweli, huruma ya Mungu kwa namna alivyofuta dhambi zetu zote na kutuweka huru, lakini pia kuonja msamaha wa kweli.” 

Askofu alisema kwa mujibu wa Injili ya Yohana kama inavyosimulia mateso hayo-Yesu Kristu alishtakiwa kwa makosa 3 ambayo hata hivyo hakuna hata moja lililokuwa na ukweli.

Shtaka la kwanza ni la kidini, ambapo Yesu alishtakiwa na Wayahudi kwa kujifanya Mwana wa Mungu, na shtaka la pili ni la kutamka kuwa atalivunja hekalu na kulijenga kwa siku 3, huku la tatu likiwa ni la kisiasa-kesi ya uhaini kwa yeye kujifanya Mfalme 
wa Wayahudi.

” Mashtaka yote haya ni ya uongo, yalilenga kupakaziana, kubambikiana kesi na kuchafuana”, alisema Mapunda huku akisisitiza kuwa mambo ya nyakati zile mpaka sasa bado yapo hata kwenye  jamii inayotuzunguka.

Alisema nyakati hizi mambo ya kuchafuana kwenye mitandao na kubambikiana kesi kwa uongo bado yapo kiasi cha baadhi ya watu kuendelea hata sasa kuozea gerezani kwa kuoneana tu Mapunda alisisitiza kwamba kilichomuua Yesu Kristu kwa mujibu wa Nabii Isaya ni dhambi na uovu wa binadamu.

Alisema kifo cha Yesu msalabani ni mapenzi ya Mungu kwa wanadamu kama chimbuko la kosa lenye heri lililofanywa na Adamu na Eva.

Hata hivyo alisisitiza kifo cha Yesu msalabani ni njia iliyompendeza Mungu kwa kuchukua uamuzi mgumu wa kumtuma mwanaye ili aje atusafishe dhambi zetu.

“Kwa tukio la leo na daima msalaba ni fahari yetu, ni mti wa uzima, mti wa wokovu na kwamba wakristu tunapaswa kujivunia msalaba,” alisema Askofu Mapunda.

Hata hivyo, katika jitihada za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa corona waumini wa kanisa hilo jana waliabudu na kusujudu msalaba huo mtakatifu kwa tendo la kuinama kwa unyenyekevu tofauti na kuubusu kwa mdomo kama ilivyozoeleka huko nyuma.

:
CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )