Aliyekamatwa na mzigo wa Bilioni 1.5 matatani “alitaka kutoa Milioni 300”

 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameagizwa kuundwa kwa Kamati Maalumu itakayojumuisha viongozi wa vyombo vya usalama ili kuchunguza sakata la mtuhumiwa aliyekamatwa na nyavu haramu za kuvulia mazao ya samaki zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5.

Mongella ametoa agizo hilo Alhamisi Aprili 09, 2020 alipofika katika Kituo cha Polisi Nyakato jijini Mwanza akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ili kujionea nyavu hizo haramu kufuatia uwepo wa taarifa za mtuhumiwa huyo aliyekamatwa Aprili 04, 2020 kuomba kuachiwa huru kwani yuko tayari kulipa faini ya shilingi milioni 300.
#BMGHabari
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akijionea moja ya nyavu haramu za kuvulia mazao ya samaki (timba) zilizokamatwa zikiwa zimehifadhiwa katika nyumba moja iliyopo Mtaa wa Nyasaka Manispaa ya Ilemela.
 Nyavu hizo haramu zilikamatwa kwa ushirikiano baina ya maafisa wa rasilimali za Uvuvi pamoja na vyombo vya usalama.

CATEGORIES
Share This

COMMENTS

Wordpress (0)
Disqus ( )