KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlingano wilayani Muheza Waziri Mohamed ambaye pia ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM)
KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza wilayani Muheza Waziri Mohamed amewataka vijana wilayani humo kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli.
Waziri ambaye pia ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) aliyasema hayo wakati aliofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mlingano Jimbo la Muheza aliyoijenga kwa kutumia kiasi cha milioni 7.
Amejitolea kujenga ofisi hiyo kutokana na kwamba kata hiyo kutokuwa nayo kwa muda mrefu na hivyo kuona haja ya kuhakikisha ujenzi huo unafanyika ili kuwawezesha viongozi kutekeleza wajibu wao wa kukijenga chama hicho.
Aidha alisema pia iwapo vijana watatumia muda wao kufikiria namna ya kujikita kwenye uanzishwaji wa viwanda hivyo utawasaidia kuweza kujiajiri na kuweza kuisaidia jamii kwa kutoa ajira kwa wenzao na hivyo kuchangia pato la mkoa na Taifa kwa ujumla.
“Lakini pia vijana wenzangu tuunge mkono juhudi za serikali kwa kushiriki kwenye miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yetu kwa kujitoa na hivyo kuchochea kasi ya ukuaji maendeleo katika jamii zinazotuzunguka “Alisema.



Muonekano wa Jengo la Ofisi ya CCM kata ya Mlingano wilayani Muheza ambalo limejengwa na KATIBU Mwenezi wa Kata ya Mlingano Jimbo la Muheza ambaye pia ni Katibu Hamasa Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed Waziri kwa asilimia 90 ambapo mpaka kukamilika kwake ametumia kiasi cha milioni 7.4
Share To:

Post A Comment: