Naibu
waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati
akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari
za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika
kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu
waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifatilia jambo wakati wa
kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za
viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika
kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI Dkt Margaret
Mollel wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kongamano la Kimataifa
la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za
binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara
litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano
la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa
afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la
sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha 220919
Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI imekuwa kitovu cha kuunda mifumo mizuri inayosimamia na kudhibiti Biashara ya Viuatilifu.
Zipo
baadhi ya nchi za Afika kusini mwa Jangwa la sahara ambazo bado
hazijatengeneza mifumo mizuri ya Kisheria na sera za kusimamia biashara
za viuatilifu.
Naibu
waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei,
2019 Jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi
kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na
mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara
litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI.
Mhe
Mgumba ameipongeza Taasisi hiyo ya TPRI kwa kushirikiana na wadau
wengine kwa kuandaa kongamano hilo Kwani ni sehemu ya kuwajengea uwezo
wadau mbalimbali ili waweze kuhakikisha kuwa Visumbufu (Pests) haviwi kikwazo katika
kutimiza azma ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais
John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda na kufikia uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema
kuwa umuhimu wa viuatilifu katika kuzalisha mazao ni jambo la wazi na
muhimu katika nchi za Ukanda wa kusini mwa Afrika na maeneo mengine
duniani hivyo kongamano hilo litakuwa chachu na taswira chanya katika
maendeleo ya kilimo nchini.
Alisema
matumizi ya viuatilifu kwa tafsiri ya wengi ni kupata mazao mengi na
hivyo mapato ya kutosha na kupata uhakika wa chakula. “Suala
la madhara ya viuatilifu hivi kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa
mazingira wengi hawalipi kipaumbele na hawaoni kwamba ni tatizo. Tatizo
linakuwa kubwa zaidi pale ambapo wengi wanatumia viuatilifu bila
kuzingatia maelekezo ya watengenezaji” Alikaririwa Mhe Hasunga
Kadhalika alisema, Visumbufu vya mazao husababisha upotevu wa karibia ya nusu ya
mazao katika Bara la Afrika na nchi zinazoendelea hivyo Bara la Afrika
likiwa linakusudia kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya watu wake
ambao wanaongezeka kwa kasi, hivyo ni lazima wakulima watumie mbinu
mbalimbali za kupambana na visumbufu vya mazao.
“Ingawa
viuatilifu vimeleta mafanikio makubwa sana duniani katika kupambana na
visumbufu vya mazao, visumbufu vya mifugo na binadamu, pia vinasababisha
madhara kwa binadamu na mazingira kwa upande mwingine” Alikaririwa Mhe
Mgumba
Aidha,
alisisitiza kuwa katika Bara la Afrika tatizo ni kubwa zaidi kuliko
maeneo mengine duniani kutokana na uwepo wa matumizi ya viuatilifu hata
vile ambavyo vimepigwa marufuku maeneo mengine duniani hivyo kuhisiwa
kusababisha madhara kwa maelfu ya watu wengi.
Alisema
kuwa matumizi ya viuatilifu au biashara zinazohusiana na viuatilifu
zinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa viuatilifu au
kwa jamii na vile vile kusababisha uchafuzi wa mazingira pale ambapo
viuatilifu havijatumika kwa njia zilizo sahihi na salama.
Tanzania kuna sheria mbili zinazoongoza katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.
Sheria hizi ni sheria ya udhibiti
wa visumbufu vya mimea Namba 13 ya Mwaka 1997 (Plant Protection Act No.
13 of 1997) na kanuni zake za mwaka 1999. Na sheria ya TPRI (The TPRI
Act. No. 18 of 1979).
Hata hivyo, Baadhi ya nchi za Kiafrika zinazotumia viuatilifu kwa wingi na zenye sheria hafifu za kusimamia matumizi ya viuatilifu, madhara
ya viuatilifu ni mengi sana kutokana na usimamizi hafifu na pia
kutokuwepo kwa huduma ya upimaji wa madhara ya viuatilifu katika afya ya
binadamu.
MWISHO
Post A Comment: