Leo Machi 29, 2018 Taasisi ya Twaweza imezindua ripoti yake ya Utafiti wa Sauti za Wananchi awamu ya 25, ambapo umeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na wabunge wa vyama vya upinzani zinaaminika kwa watu asilimia 12 pekee huku zile zinazotolewa na wabunge wa chama tawala cha CCM zinaaminika kwa wananchi asilimia 26.Kwenye ripoti hiyo ya Twaweza imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na Rais zinaaminika kwa asilimia 70 ya wananchi huku zinazotolewa na Makamu wa Rais zikiaminika kwa asilimia 64.

Kwa maana nyingine, asilimia 16 ya wananchi hawaamini kabisa taarifa zinazotolewa na wabunge wa upinzani huku asilimia 6 pekee ya wananchi hawaamini taarifa zinazotolewa na wabunge wa CCM.

Aidha ripoti hiyo pia imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na wanachama wa vyama vya upinzani zinaaminika kwa asilimia 9 ya wananchi huku wanachama wa chama tawala cha CCM taarifa zao zikiaminika kwa asilimia 27.

Kwa upande mwingine ripoti hiyo imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na wenyeviti wa mitaa na vijiji zinaaminika kwa asilimia 30 ya wananchi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: